Surat Al-Baqarah, aya 218

2:218

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أُوْلَٰٓئِكَ يَرۡجُونَ رَحۡمَتَ ٱللَّهِۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ٢١٨

Innal-ladhīna āmanū walladhīna hājarū wajāhadū fī sabīlillāhi ulā'ika yarjūna rahmatallāhi wallāhu ghafūrur rahīm

Hakika wale walio amini na wale walio hama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanao taraji rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. 218

Maelezo ya chini

218 Wenye kuamini imani ya kweli hata wakahama kwa ajili ya kuinusuru Dini na kwa ajili ya Jihadi ili Dini ienee hao wanangojea thawabu kubwa za Mwenyezi Mungu. Na ikiwa wamefanya kasoro kitu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, anasamehe dhambi, Mwenye kurehemu, anawarehemu waja wake kwa uwongofu na kuwalipa.