سَلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ كَمۡ ءَاتَيۡنَٰهُم مِّنۡ ءَايَةِۭ بَيِّنَةٖۗ وَمَن يُبَدِّلۡ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ٢١١
Sal banī isrā'īla kam ātaynāhum min āyati bayyinatin waman yubaddil ni'matallāhi mim ba'di mā jā'athu fa innallāha shadīdul-'iqāb
Waulize Wana wa Israili: Tumewapa ishara ngapi zilizo wazi? Na anaye zibadili neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. 211
Maelezo ya chini
211 Waulize Wana wa Israili tumewaletea dalili ngapi za kukata za kuthibitisha ukweli wa Mtume! Na hayo ni neema ya kutaka kuwaongoa wamwendee Mwenyezi Mungu. Lakini wapi! Walizikataa hizo dalili na wakashikilia kuzikanusha hadi ya kuyageuza makusudio yake. Baada ya kuwa hizo dalili ni kwa ajili ya uwongofu zikawa kwa ukafiri wao ni sababu ya kuwazidisha upotovu na kutenda dhambi. Na mwenye kugeuza neema ya Mwenyezi Mungu kwa namna hii basi huyo anastahiki adhabu, na Mwenyezi Mungu hakika ni mkali wa kuadhibu.