وَإِذَا قِيلَ لَهُ ٱتَّقِ ٱللَّهَ أَخَذَتۡهُ ٱلۡعِزَّةُ بِٱلۡإِثۡمِۚ فَحَسۡبُهُۥ جَهَنَّمُۖ وَلَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ ٢٠٦
Wa idhā qīla lahut-taqillāha akhadhathul-'izzatu bil-ithmi fahasbuhū jahannamu walabi'sal-mihād
Na akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kutenda madhambi. Basi huyo inamtosha Jahannam. Paovu mno hapo kwa mapumziko. 206
Maelezo ya chini
206 Akinasihiwa amwogope Mwenyezi Mungu huzidi kupanda mori wake na akadhani kuwa hivyo unamvunjia cheo chake, akazidi kupanda madhambi na kuzidi kumchafua na kumwongeza inadi. Mtu huyo hatoshelezeki mpaka aingie Jahannam, na hayo ni makao maovu mno.