Surat Al-Baqarah, aya 135

2:135

وَقَالُواْ كُونُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰ تَهۡتَدُواْۗ قُلۡ بَلۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِـۧمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ١٣٥

Waqālū kūnū hūdan aw nasārā tahtadū qul bal millata ibrāhima hanīfan wamā kāna minal-mushrikīn

Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina. 135

Maelezo ya chini

135 Lakini wao hawaachi kuendelea katika ghasia na inda zao. Kila kikundi katika hao hudai kuwa ni dini yao wao tu ndiyo iliyo sawa. Mayahudi hukuambieni: Kuweni Mayahudi mpate kuhidika na kuongokewa kwenye njia sawa. Na Wakristo nao wanasema: Kuweni Wakristo ndio mpate kuongoka kwenye haki iliyo nyooka. Nyinyi wajibuni kuwa sisi hatufuati hii wala hii kwa sababu dini zote hizo mbili zimekwisha potoka na zimeacha ile asli yake ya kweli, na zimeingia ndani yake ushirikina (upagani), na ziko mbali kabisa na mila ya Ibrahim. Bali sisi tunaufuata Uislamu ndio ulio ifanya mila ya Ibrahim kuwa safi iliyo safika.