وَلِلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ فَأَيۡنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجۡهُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ ١١٥
Walillāhil-mashriqu wal-maghribu fa aynamā tuwallū fathamma wajhullāhi innallāha wāsi'un 'alīm
Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu. Basi kokote mnako elekea, huko Mwenyezi Mungu yupo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa na Mjuzi. 115
Maelezo ya chini
115 Ikiwa washirikina waliwazuia Waislamu kusali katika Msikiti Mtakatifu wa Makka, hawatoweza kuwazuia kusali na kumuabudu Mwenyezi Mungu. Kwani jiha zote na pande zote za dunia ni za Mwenyezi Mungu. Na hakika bila ya shaka Mwenyezi Mungu anampokelea Muislamu Sala zake, na anamkabili kwa radhi yake pande zote anapo fanya ibada yake. Kwani Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, hawadhikishi waja wake, na Yeye ni Mwenye kuijua vyema niya ya mwenye kumuelekea.