أَمۡ تُرِيدُونَ أَن تَسۡـَٔلُواْ رَسُولَكُمۡ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبۡلُۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ ٱلۡكُفۡرَ بِٱلۡإِيمَٰنِ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ ١٠٨
Am turīdūna an tas'alū rasūlakum kamā su'ila mūsā min qablu waman yatabaddalil-kufra bil-īmāni faqad dalla sawā'as-sabīl
Au mnataka kumwomba Mtume wenu kama alivyo ombwa Musa zamani? Na anaye badilisha Imani kwa ukafiri bila ya shaka huyo ameipotea njia iliyo sawa. 108
Maelezo ya chini
108 Na kwa kule kumtaka kwenu Mtume wenu Muhammad miujiza fulani pengine ilikuwa mnawaiga Wana wa Israili wa zama za Musa, walipo mtaka awaletee miujiza maalumu. Kutaka kwenu huku kunaficha nyuma yake inda na kumili kwenye ukafiri, kama kulivyo kuwa kule kutaka kwa Wana wa Israili kumtaka Mtume wao. Na mwenye kufuata nyayo za inda na ukafiri akaacha usafi wa kutaka Haki na Imani basi huyo ameipotea Njia iliyo sawa iliyo nyooka.