Surat Al-A'raf, aya 79

7:79

فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُحِبُّونَ ٱلنَّٰصِحِينَ ٧٩

Fatawallā 'anhum waqāla yāqawmi laqad ablaghtukum risālata rabbī wanasahtu lakum walākil lā tuhibbūnan-nāsihīn

Basi Swaleh akwaacha na akasema: Enyi watu wangu! Nilikufikishieni Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye nasaha. 79

Maelezo ya chini

79 Na kabla ya kuwateremkia adhabu hiyo ndugu yao Swaleh aliwaachilia mbali (kwa kukata tamaa nao), akawaambia: Enyi watu wangu! Mimi nimekufikishieni amri na makatazo ya Mola Mlezi wangu. Na nimekusafieni nasaha yangu, lakini nyinyi kwa ushindani wenu na ushupavu wenu, mmekuwa hamumpendi anaye kunasihini!