Surat Al-A'raf, aya 51

7:51

ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَهُمۡ لَهۡوٗا وَلَعِبٗا وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ فَٱلۡيَوۡمَ نَنسَىٰهُمۡ كَمَا نَسُواْ لِقَآءَ يَوۡمِهِمۡ هَٰذَا وَمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَجۡحَدُونَ ٥١

Alladhīnat-takhadhū dīnahum lahwan wala'iban wagharrathumul-hayawātud-dunyā fal-yawma nansāhum kamā nasū liqā'a yawmihim hādhā wamā kānū bi'āyātinā yajhadūn

Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo Sisi tunawasahau kama walivyo usahau mkutano wa Siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu. 51

Maelezo ya chini

51 Hawa makafiri ndio ambao hawakufanya juhudi kutafuta Dini ya Haki, lakini ikawa dini yao ni kufuata pumbao na matamanio, ndio pumbao la kujipumbazia na upuuzi wa kuchezea, na maisha ya dunia na anasa zake zikawakhadaa, wakadhania hayo tu ndiyo maisha, na wakasahau kukutana nasi! Basi Siku ya Kiyama Sisi tutawasahau. Na wao hawato istarehea Pepo, na watauonja Moto, kwa sababu ya sahau yao kuisahau Siku ya Kiyama, na kuzikanusha Ishara zenye kubainika wazi, zinazo thibitisha Haki.