Surat Al-A'raf, aya 50

7:50

وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ أَنۡ أَفِيضُواْ عَلَيۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ أَوۡ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُۚ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ ٥٠

Wanādā ashābun-nāri ashābal-jannati an afīdū 'alaynā minal-mā'i aw mimmā razaqakumullāhu qālū innallāha harramahumā 'alal-kāfirīn

Na watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi: Tumimieni maji, au chochote alicho kuruzukuni Mwenyezi Mungu. Nao watasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameviharimisha hivyo kwa makafiri, 50

Maelezo ya chini

50 Na watu wa Motoni watawanadia watu wa Peponi kwa kuwaambia: Hebu twachilieni maji kidogo yatumiminikie sisi, au tugaieni kitu katika vyakula na mavazi na starehe nyengine alizo kupeni Mwenyezi Mungu Mtukufu! Nao watu wa Peponi watawajibu: Sisi hatuwezi kufanya hayo, kwa sababu Mwenyezi Mungu amezuia vyote hivyo wasipate watu wapinzani, walio mkanusha Yeye na neema zake katika dunia.