وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ نَزۡغٞ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ٢٠٠
Wa immā yanzaghannaka minash-shaytāni nazghun fasta'idh billāhi innahū samī'un 'alīm
Na uchochezi wa Shet'ani ukikuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi, Mjuzi. 200
Maelezo ya chini
200 Na Shetani akikuchochea kwa wasiwasi ili apate kukuachisha ulio amrishwa, kama vile kukasirika kwa kukushikilia kwao mambo ya shari, basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu akuepushe naye huyo Shetani. Kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na kujua kila linalo tokea.