أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٌ ١٨٤
Awalam yatafakkarū mā bisāhibihim min jinnatin in huwa illā nadhīrum mubīn
Je, hawafikiri? Huyu mwenzao hana wazimu. Hakuwa yeye ila ni mwonyaji aliye dhaahiri. 184
Maelezo ya chini
184 Wao wameanza kwa kukadhibisha, wala hawakuzingatia yale anayo waitia kwayo Mtume, na hoja anazo zitoa. Bali wakamsingizia kuwa ni mwendaazimu, na hali hana wazimu chochote. Yeye huyu ni mwenye kuwaonya wasifikiwe na adhabu ya ushirikina wao. Na onyo lake liwazi, la dhaahiri.