Surat Al-A'raf, aya 162

7:162

فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ قَوۡلًا غَيۡرَ ٱلَّذِي قِيلَ لَهُمۡ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَظۡلِمُونَ ١٦٢

Fabaddalal-ladhīna zalamū minhum qawlan ghayral-ladhī qīla lahum fa arsalnā 'alayhim rijzam minas-samā'i bimā kānū yazlimūn

Lakini walio dhulumu miongoni mwao walibadilisha kauli, sio ile waliyo ambiwa. Basi tukawapelekea adhabu kutoka mbinguni kwa vile walivyo kuwa wakidhulumu. 162

Maelezo ya chini

162 Lakini waliikhalifu amri ya Mola wao Mlezi, wakasema kwa udhalimu maneno sio walio ambiwa, kwa kusudi ya kumkejeli Musa. Basi tukawateremshia adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya kuendelea kwao na udhalimu na kukiuka mpaka.