Surat Al-A'raf, aya 129

7:129

قَالُوٓاْ أُوذِينَا مِن قَبۡلِ أَن تَأۡتِيَنَا وَمِنۢ بَعۡدِ مَا جِئۡتَنَاۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُهۡلِكَ عَدُوَّكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ ١٢٩

Qālū ūdhīnā min qabli an ta'tiyanā wamim ba'di mā ji'tanā qāla 'asā rabbukum an yuhlika 'aduwwakum wayastakhlifakum fil-ardi fayanzura kayfa ta'malūn

Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi. 129

Maelezo ya chini

129 Wakasema wale watu kwa huzuni na unyonge: Sisi tulipata maudhi zamani kutoka kwa Firauni kabla hujatujia, na hivi sasa tena baada ya kuja kwako. Musa akawafungulia mlango wa matarajio mema kwa kuwaambia: Hakika linalo tarajiwa kwa fadhila za Mola wenu Mlezi ni kumteketeza adui yenu, aliye kufanyeni watumwa na akakuteseni kwa dhulma yake, na akujaalieni nyinyi ndio wa kuimiliki ardhi aliyo kuahidini. Yeye Subhanahu, Aliye takasika, anayajua mnayo yatenda baada ya kukuwekeni huku. Je, mtaishukuru neema au mtaikufuru? Na mtatenda mema katika nchi au mtafanya fisadi? Hayo ili apate kukulipeni duniani na Akhera kwa mujibu wa mtendayo.