Surat Al-A'raf, aya 128

7:128

قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ ١٢٨

Qāla mūsā liqawmihista'īnū billāhi wasbirū innal-arda lillāhi yūrithuhā man yashā'u min 'ibādihī wal-'āqibatu lil-muttaqīn

Musa akawaambia watu wake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu. Naye humrithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho ni wa wachamngu. 128

Maelezo ya chini

128 Na hapo Musa aliona kama dalili za huzuni katika watu wake, basi akawatia nguvu katika azma yao. Akawambia: Mtakeni Mwenyezi Mungu msaada na kukuungeni mkono. Na kuweni imara, wala msifazaike. Kwani ardhi yote imo katika nguvu za uwezo wa Mwenyezi Mungu na ufalme wake. Humrithisha amtakaye katika waja wake, wala si ya Firauni. Na mwisho mwema wataupata wale wanao mcha Mwenyezi Mungu kwa kushikamana naye na kuzikamata hukumu zake.