قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ ١٠٩
Qālal-mala'u min qawmi fir'awna inna hādhā lasāhirun 'alīm
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi. 109
Maelezo ya chini
109 Musa alipo ionyesha Ishara ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, zilitibuka roho za wapambe wa Firauni na waheshimiwa wa kaumu yake, wakasema katika kujipendekeza kwa Firauni na kumtetea: Hakika huyu ni bingwa katika ilimu ya uchawi, wala hii si Ishara itokayo kwa Mwenyezi Mungu!!