وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۢ بَعۡدُ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ مَعَكُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ مِنكُمۡۚ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ ٧٥
Walladhīna āmanū mim ba'du wahājarū wajāhadū ma'akum fa ulā'ika minkum wa ulul-arhāmi ba'duhum awlā biba'din fī kitābillāhi innallāha bikulli shay'in 'alīm
Na watakao amini baadaye na wakahajiri, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni katika nyinyi. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. 75
Maelezo ya chini
75 Na walio amini baada ya wale wa mwanzo, na mwishoe wakahama nao, na wakapigana Jihadi pamoja na walio tangulia, basi hao ni katika nyinyi, kwa mkusanyiko wa Muhaajirina (Walio hama Makka) na Ansari (walio msaidia Mtume, watu wa Madina). Hao wanastahiki ulinzi na haki kama ziliopo baina ya nyinyi kwa nyinyi. Na walio kuwa wame nasibiana katika Waumini - juu ya urafiki wa Imani -wana urafiki zaidi wa kuwa ni jamaa. Basi hao wanazidiana katika mapenzi, na mali, na kusaidiana, na kuungana mkono. Na Mwenyezi Mungu ameyabainisha hayo katika Kitabu chake. Naye ni Mwenye kujua kila kitu.