وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٍۚ إِلَّا تَفۡعَلُوهُ تَكُن فِتۡنَةٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَفَسَادٞ كَبِيرٞ ٧٣
Walladhīna kafarū ba'duhum awliyā'u ba'din illā taf'alūhu takun fitnatun fil-ardi wafasādun kabīr
Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika nchi na fisadi kubwa. 73
Maelezo ya chini
73 Na walio kufuru wao ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Na wao husaidiana kwa mambo ya upotovu, na wanaungana mkono kukufanyieni nyinyi uadui. Basi nyinyi msifanye nao urafiki. Mkikhaalifu, yaani mkenda kinyume na haya mkawafanya ni wenzenu itaingia fitna katika safu zenu, na utakuwa uharibifu mkubwa katika nchi.