Surat Al-Anfal, aya 72

8:72

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَواْ وَّنَصَرُوٓاْ أُوْلَٰٓئِكَ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يُهَاجِرُواْ مَا لَكُم مِّن وَلَٰيَتِهِم مِّن شَيۡءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُواْۚ وَإِنِ ٱسۡتَنصَرُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ فَعَلَيۡكُمُ ٱلنَّصۡرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٞۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ٧٢

Innal-ladhīna āmanū wahājarū wajāhadū bi amwālihim wa anfusihim fī sabīlillāhi walladhīna āwaw wwanasarū ulā'ika ba'duhum awliyā'u ba'din walladhīna āmanū walam yuhājirū mā lakum min walāyatihim min shay'in hattā yuhājirū wa inistansarūkum fid-dīni fa'alaykumun-nasru illā 'alā qawmi baynakum wabaynahum mīthāqun wallāhu bimā ta'malūna basīr

Hakika wale walio amini na wakahama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, na wale walio toa mahala pa kukaa, na wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walio amini lakini hawakuhama, nyinyi hamna waajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipo kuwa juu ya watu ambao yapo mapatano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. 72

Maelezo ya chini

72 Hakika walio isadiki Haki na wakaikubali hukumu yake, wakahama Makka, wakapigana Jihadi kwa mali yao na roho zao, na wale walio wapa makaazi wakimbizi ugenini, wakamsaidia Mtume wa Mwenyezi Mungu, wanapigana vita na wale wanao wapiga vita. Wanamfanyia uadui anao wafanyia uadui. Wao kwa wao wanasaidia kuunga mkono Haki, na kutukuza Neno la Mwenyezi Mungu. Na wale wasio hama, haijathibiti kupata ulinzi na msaada wa Waumini, mpaka wahajiri. Lakini wakikutakeni muwanusuru na wanao wakandamiza katika Dini, basi wanusuruni. Wakikutakeni muwasaidie dhidi ya watu ambao mna mapatano nao, na wala hawakuvunja mapatano hayo, basi msiwakubalie. Na Mwenyezi Mungu anayaona myatendayo, hana kinacho fichika kwake. Basi simameni kwenye mipaka yake msije mkatumbukia katika adhabu yake.