يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ حَرِّضِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ عَلَى ٱلۡقِتَالِۚ إِن يَكُن مِّنكُمۡ عِشۡرُونَ صَٰبِرُونَ يَغۡلِبُواْ مِاْئَتَيۡنِۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّاْئَةٞ يَغۡلِبُوٓاْ أَلۡفٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ ٦٥
Yā'ayyuhan-nabiyyu harridil-mu'minīna 'alal-qitāli in yakum minkum 'ishrūna sābirūna yaghlibū mi'atayni wa in yakum minkum mi'atun yaghlibū alfam minal-ladhīna kafarū bi annahum qawmul lā yafqahūn
Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo kati yenu ishirini wanao subiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja katika walio kufuru. Kwa sababu wao ni watu wasio fahamu. 65
Maelezo ya chini
65 Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani kwa ajili ya kulinyanyua Neno la Mwenyezi Mungu, na wapendezeshe kwa yatayo wafwatia katika kheri ya dunia na Akhera watayo ipata, ili nafsi zao ziingie nguvu. Nayo ikiwa wapo kati yenu watu ishirini walio shikamana na Imani na subira na ut'iifu, basi watawashinda makafiri mia mbili. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasio fahamu ukweli wa mambo, kwani hawana Imani, wala subira, wala tamaa ya kupata thawabu.