وَٱقۡتَرَبَ ٱلۡوَعۡدُ ٱلۡحَقُّ فَإِذَا هِيَ شَٰخِصَةٌ أَبۡصَٰرُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَٰوَيۡلَنَا قَدۡ كُنَّا فِي غَفۡلَةٖ مِّنۡ هَٰذَا بَلۡ كُنَّا ظَٰلِمِينَ ٩٧
Waqtarabal-wa'dul-haqqu fa idhā hiya shākhisatun absārul-ladhīna kafarū yāwaylanā qad kunnā fī ghaflatim min hādhā bal kunnā zālimīn
Na miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatapo kodoka macho ya walio kufuru (na watasema:) Ole wetu! Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu. 97
Maelezo ya chini
97 Na ikakaribia miadi iliyo haina budi kutimizwa, nayo ni Siku ya Kiyama, wakawa wale walio kufuru wanakutikana wakikodoa macho yao kwa wingi wa kitisho, wakipiga makelele kusema: Kitisho gani hichi cha kutuangamiza! Hakika sisi tulighafilika na Siku hii. Bali tulikuwa ni wenye kujidhulumu nafsi zetu kwa ukafiri na inda.