Surat Al-Anbiya, aya 80

21:80

وَعَلَّمۡنَٰهُ صَنۡعَةَ لَبُوسٖ لَّكُمۡ لِتُحۡصِنَكُم مِّنۢ بَأۡسِكُمۡۖ فَهَلۡ أَنتُمۡ شَٰكِرُونَ ٨٠

Wa'allamnāhu san'ata labūsil lakum lituhsinakum mim ba sikum fahal antum shākirūn

Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika kupigana kwenu. Je! Mtakuwa wenye kushukuru? 80

Maelezo ya chini

80 Tukamfundisha Daud kufuma nguo za chuma, ili zikulindeni katika vita vyenu. Basi mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa neema hii aliyo kuneemesheni.