فَفَهَّمۡنَٰهَا سُلَيۡمَٰنَۚ وَكُلًّا ءَاتَيۡنَا حُكۡمٗا وَعِلۡمٗاۚ وَسَخَّرۡنَا مَعَ دَاوُۥدَ ٱلۡجِبَالَ يُسَبِّحۡنَ وَٱلطَّيۡرَۚ وَكُنَّا فَٰعِلِينَ ٧٩
Fafahhamnāhā sulaymāna wakullan ātaynā hukman wa'ilman wasakkharnā ma'a dāwūdal-jibāla yusabbihna wat-tayra wakunnā fā'ilīn
Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo. 79
Maelezo ya chini
79 Basi tulimfahamisha Suleiman hiyo fatwa. Na wote wawili tuliwapa hikima na ilimu ya maisha na mambo yake. Na tulimfanyia Daud pamoja na milima it'ii na imtakase Mwenyezi Mungu kama alivyo kuwa anamtakasa yeye Daud na kila lisio kuwa linamwelekea Mwenyezi Mungu. Na kadhaalika tuliwafanya ndege hivyo hivyo wamsabihi Mwenyezi Mungu pamoja naye. Na tulifanya hayo kwa uweza wetu usio shindika.