وَمَآ أَرۡسَلۡنَا قَبۡلَكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ ٧
Wamā arsalnā qablaka illā rijālan nūhī ilayhim fas'alū ahladh-dhikri in kuntum lā ta'lamūn
Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui. 7
Maelezo ya chini
7 Ewe Nabii! Kabla yako wewe hatukuwatumia watu ila watu wa kibinaadamu vile vile, ambao tuliwafunulia Dini waifikishe kwa watu. Basi, enyi mnao kataa! Waulizeni wanazuoni wajuao ilimu za Vitabu vilivyo teremka, ikiwa nyinyi hamyajui hayo.