Surat Al-Anbiya, aya 48

21:48

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ ٱلۡفُرۡقَانَ وَضِيَآءٗ وَذِكۡرٗا لِّلۡمُتَّقِينَ ٤٨

Walaqad ātaynā mūsā wahārūnal-furqāna wadiyā'an wadhikral lil-muttaqīn

Na kwa yakini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi, na mwangaza, na makumbusho kwa wachamngu, 48

Maelezo ya chini

48 Na Musa na Haaruni tuliwapa Taurati ya kupambanua baina ya kweli na uwongo, na halali na haramu. Na juu ya hivyo hiyo ni nuru ya kuwaongoa watu wafuate njia ya kheri na uwongozi mwema, na ni kumbusho la kuwafaa wachamngu...