وَكَمۡ قَصَمۡنَا مِن قَرۡيَةٖ كَانَتۡ ظَالِمَةٗ وَأَنشَأۡنَا بَعۡدَهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ ١١
Wakam qasamnā min qaryatin kānat zālimatan wa ansha'nā ba'dahā qawman ākharīn
Na mingapi katika miji iliyo kuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawasimamisha baada yao watu wengine. 11
Maelezo ya chini
11 Na wengi katika watu wa miji tuliyo iteketeza kwa sababu ya ukafiri wao na kuwakadhibisha Manabii, na baada yao tukasimamisha kaumu nyengine zenye hali bora na mwisho mwema kuliko hao.