Surat Al-Anbiya, aya 10

21:10

لَقَدۡ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ كِتَٰبٗا فِيهِ ذِكۡرُكُمۡۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ ١٠

Laqad anzalnā ilaykum kitāban fīhi dhikrukum afalā ta'qilūn

Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii? 10

Maelezo ya chini

10 Sisi hakika tumekuteremshieni Kitabu. Ndani yake yamo mawaidha ya kuwakumbusheni ikiwa mtakisoma na mtayatenda yaliyomo ndani yake. Basi huwaje mkakipuuza na mkakikataa? Je, inda na upumbavu umefika hadi ya kukufikisheni hali hii mlio nayo, mkawa hamuelewi lipi lenye manufaa nanyi mkalikimbilia?