وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۖ وَيَوۡمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُۚ قَوۡلُهُ ٱلۡحَقُّۚ وَلَهُ ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ ٧٣
Wahuwal-ladhī khalaqas-samāwāti wal-arda bil-haqqi wayawma yaqūlu kun fayakūnu qawluhul-haqqu walahul-mulku yawma yunfakhu fis-sūri 'ālimul-ghaybi wash-shahādati wahuwal-hakīmul-khabīr
Naye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litapo pulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Naye ndiye Mwenye hikima na Mwenye khabari. 73
Maelezo ya chini
73 Na ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akasimamia uumbaji wake kwa Haki na hikima. Na wakati wowote Mwenyezi Mungu akitaka kiwe kitu kinakuwa papo hapo. Vitu huwa kwa neno: "Kuwa". Na kila neno lake ni la kweli na la haki. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye uweza wa kutenda usio na ukomo Siku ya Kiyama, siku litapo pulizwa barugumu la kutangazwa ufufuo. Naye, Subhanahu, ndiye Mwenye kutulia juu ya ujuzi wake wa mambo yaliyo fichikana na yanayo onekana. Na ndiye anaye endesha mambo yake yote kwa hikima, na ndiye Mwenye kukusanya katika ujuzi wake mambo yaliyo fichikana na mambo yaliyo dhihiri.