وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۖ وَيُرۡسِلُ عَلَيۡكُمۡ حَفَظَةً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ تَوَفَّتۡهُ رُسُلُنَا وَهُمۡ لَا يُفَرِّطُونَ ٦١
Wahuwal-qāhiru fawqa 'ibādihī wayursilu 'alaykum hafazatan hattā idhā jā'a ahadakumul-mawtu tawaffathu rusulunā wahum lā yufarritūn
Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na hukupelekeeni waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri. 61
Maelezo ya chini
61 Naye ndiye Mwenye kushinda kwa uwezo wake, aliye tukuka kwa ufalme wake juu ya waja wake, na anaye kupelekeeni Malaika wa kudhibiti kila vitendo vyenu, mpaka ufike mwisho wa kila mmoja wenu, ishikwe roho yake na Malaika wetu tunao wapeleka kwa kazi hiyo. Na wao hao Malaika hawafanyi taksiri katika kazi walio wakilishwa kuitenda.