وَهُوَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُم بِٱلَّيۡلِ وَيَعۡلَمُ مَا جَرَحۡتُم بِٱلنَّهَارِ ثُمَّ يَبۡعَثُكُمۡ فِيهِ لِيُقۡضَىٰٓ أَجَلٞ مُّسَمّٗىۖ ثُمَّ إِلَيۡهِ مَرۡجِعُكُمۡ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ٦٠
Wahuwal-ladhī yatawaffākum billayli waya'lamu mā jarahtum bin-nahāri thumma yab'athukum fīhi liyuqdā ajalum musamman thumma ilayhi marji'ukum thumma yunabbi'ukum bimā kuntum ta'malūn
Naye ndiye anaye kufisheni usiku, na anakijua mlicho fanya mchana. Kisha Yeye hukufufueni humo mchana ili muda ulio wekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu, na tena akwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. 60
Maelezo ya chini
60 Na Yeye ndiye anakulazeni usiku, na anakuamsheni mchana. Na anajua mnayo yachuma, mpaka utimie muda wa kumfikia kila mmoja wenu ajali yake duniani ya kufa. Kisha Siku ya Kiyama mtarejeshwa nyote nyinyi kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Tena atakwambieni a'mali zenu mlizo tenda duniani, njema au mbaya, na akulipeni kwazo.