وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلِتَسۡتَبِينَ سَبِيلُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ ٥٥
Wakadhālika nufassilul-āyāti walitastabīna sabīlul-mujrimīn
Na ndio hivi tunavyo zieleza Ishara ili ibainike njia ya wakosefu. 55
Maelezo ya chini
55 Na kwa mfano wa bayana hiyo iliyo wazi, tunaweka wazi dalili mbali mbali, ipate kudhihiri njia ya Haki wanayo ipitia Waumini, na ibainishe njia ya upotovu wanayo ipitia makafiri.