قُلۡ إِنِّي نُهِيتُ أَنۡ أَعۡبُدَ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۚ قُل لَّآ أَتَّبِعُ أَهۡوَآءَكُمۡ قَدۡ ضَلَلۡتُ إِذٗا وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُهۡتَدِينَ ٥٦
Qul innī nuhītu an a'budal-ladhīna tad'ūna min dūnillāhi qul lā attabi'u ahwā'akum qad dalaltu idhan wamā ana minal-muhtadīn
Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu. Sema: mimi sifuati matamanio yenu. Hivyo nitakuwa nimepotea, na sitakuwa miongoni mwa walio ongoka. 56
Maelezo ya chini
56 Ewe Nabii! Waambie hawa makafiri: Hakika Mwenyezi Mungu amenikataza kuwaabudu hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Basi mimi sifuati matamanio yenu. Kwani nikikufuateni nitakuwa nimekengeuka kuiacha Haki, na sitokuwa katika waongofu!