وَإِذَا جَآءَكَ ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِـَٔايَٰتِنَا فَقُلۡ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡۖ كَتَبَ رَبُّكُمۡ عَلَىٰ نَفۡسِهِ ٱلرَّحۡمَةَ أَنَّهُۥ مَنۡ عَمِلَ مِنكُمۡ سُوٓءَۢا بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَصۡلَحَ فَأَنَّهُۥ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ٥٤
Wa idhā jā'akal-ladhīna yu'minūna bi'āyātinā faqul salāmun 'alaykum kataba rabbukum 'alā nafsihir-rahmata annahū man 'amila minkum sū'ā bijahālatin thumma tāba mim ba'dihī wa aslaha fa annahū ghafūrur rahīm
Na wanapo kujia wanao ziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! Amani iwe juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakaye fanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. 54
Maelezo ya chini
54 Na wakikujia wanao isadiki Qur'ani waambie kwa kuwahishimu: Assalamu Alaikum, Amani juu yenu. Nakubashirieni rehema kunjufu ya Mwenyezi Mungu, ambayo amejilazimisha Yeye Mwenyewe, kwa fadhila yake, na ambayo inahukumu kuwa yeyote katika nyinyi akitenda ubaya bila ya kuzingatia matokeo yake, kisha akarejea kwa Mwenyezi Mungu naye amejuta, ametubu, na akatengeneza a'mali zake, basi Mwenyezi Mungu atamghufiria, kwani Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghfira, na mkunjufu wa rehema.