Surat Al-An'am, aya 53

6:53

وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لِّيَقُولُوٓاْ أَهَٰٓؤُلَآءِ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنۢ بَيۡنِنَآۗ أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَعۡلَمَ بِٱلشَّٰكِرِينَ ٥٣

Wakadhālika fatannā ba'dahum biba'dil liyaqūlū ahā'ulā'i mannallāhu 'alayhim mim bayninā alaysallāhu bi a'lama bish-shākirīn

Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanao shukuru? 53

Maelezo ya chini

53 Na kwa majaribio kama haya ambayo ndio ada yetu kuyatenda, tukawafanyia mtihani walio takabari kwa kuwatanguliza wanyonge wawe mbele kusilimu; wapate kusema wenye kiburi, wanao pinga, wakifanya kejeli: Hivyo ni hawa mafakiri ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwetu sote kwa kuwapa hiyo kheri aliyo waahidi Muhammad? Hakika hawa mafakiri wanaijua neema ya Mwenyezi Mungu juu yao kwa kuwapa tawfiki ya kuifikia Imani, na kwa hivyo wanamshukuru. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua zaidi nani anashukuru fadhila yake na neema yake.