قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ أَوۡ أَتَتۡكُمُ ٱلسَّاعَةُ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَدۡعُونَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٤٠
Qul ara'aytakum in atākum 'adhābullāhi aw atatkumus-sā'atu aghayrallāhi tad'ūna in kuntum sādiqīn
Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni hiyo Saa - mtamwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli? 40
Maelezo ya chini
40 Ewe Nabii! Waambie hawa makafiri: Nambieni, ikikujieni adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu hapa duniani, au ikikujieni Kiyama kwa vitisho vyake, mtamuelekea yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu mkimnyenyekea wakati huo akufaeni kwa lolote, kama nyinyi mnasema kweli katika kumuabudu kwenu asiye kuwa Mwenyezi Mungu?