Surat Al-An'am, aya 39

6:39

وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا صُمّٞ وَبُكۡمٞ فِي ٱلظُّلُمَٰتِۗ مَن يَشَإِ ٱللَّهُ يُضۡلِلۡهُ وَمَن يَشَأۡ يَجۡعَلۡهُ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ ٣٩

Walladhīna kaddhabū bi'āyātinā summun wabukmun fiz-zulumāti man yasha'illāhu yudlilhu waman yasha' yaj'alhu 'alā sirātim mustaqīm

Na walio kanusha Ishara zetu ni viziwi na mabubu waliomo gizani. Mwenyezi Mungu humwachia kupotea amtakaye, na humweka katika Njia iliyo nyooka amtakaye. 39

Maelezo ya chini

39 Na ambao hawakuzisadiki dalili zetu zinazo onyesha uwezo wetu na ukweli wa Utume wako, basi hao hawakunafiika na hisiya zao kuwawezesha kuitambua Haki. Kwa hivyo wakawa wanababaika katika upotovu wa ushirikina na inda, kama anavyo babaika kiziwi-bubu katika giza la usiku, hawezi kuepuka kuangamia. Lau kuwa watu hawa wameelekea kheri Mwenyezi Mungu angeli wawezesha wamfikie, kwani Yeye Subhanahu akitaka kumpoteza mtu kwa ufisadi wake alio ukusudia, basi humwachilia mbali na shani yake; na akitaka kumwongoa mtu kwa kuwa makusudio yake ni sawa, basi humsahilishia njia ya Imani iliyo wazi na iliyo nyooka.