وَقَالُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يُنَزِّلَ ءَايَةٗ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ٣٧
Waqālū lawlā nuzzila 'alayhi āyatum mir rabbihī qul innallāha qādirun 'alā an yunazzila āyatan walākinna aktharahum lā ya'lamūn
Na wamesema kwanini hakuteremshiwa Miujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi ? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuteremsha Miujiza lakini wengi wao hawajui 37
Maelezo ya chini
37 Na makafiri washupavu wamesema: Tunataka ateremshiwe Muhammad dalili ya kuonekana kutoka kwa Mola wake Mlezi, itayo shuhudia ukweli wa huu wito wake! Waambie, ewe Nabii: Hakika Mwenyezi Mungu anaweza kuteremsha hiyo dalili muitakayo. Lakini wengi wao hawajui nini hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuziteremsha Ishara. Na hayo hayafuati matamanio yao. Na lau kuwa Yeye akiwakubalia hilo walitakalo, na kisha wakakanusha baada yake, basi atawateketeza tu. Lakini wengi wao hawajui nini matokeo ya vitendo vyao!!