۞ إِنَّمَا يَسۡتَجِيبُ ٱلَّذِينَ يَسۡمَعُونَۘ وَٱلۡمَوۡتَىٰ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ ثُمَّ إِلَيۡهِ يُرۡجَعُونَ ٣٦
Innamā yastajībul-ladhīna yasma'ūna wal-mawtā yab'athuhumullāhu thumma ilayhi yurja'ūn
Hakika wanao kubali ni wale wanao sikia. Na ama wafu Mwenyezi Mungu atawafufua, na kisha kwake Yeye ndio watarejeshwa. 36
Maelezo ya chini
36 Hakika wanao itikia wito wa Haki ni wale wanao ukubali - wale ambao wanao sikia kwa msikio wa kufahamu na kuzingatia. Ama hao walio potoka kabisa hawanafiiki kwa wito wako, kwani wao wamo katika hukumu ya maiti. Na Mwenyezi Mungu atawafufua kutoka makaburini Siku ya Kiyama, na atawarejeza kwake awahisabu kwa waliyo yafanya.