Surat Al-An'am, aya 32

6:32

وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا لَعِبٞ وَلَهۡوٞۖ وَلَلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ ٣٢

Wamal-hayawātud-dunyā illā la'ibun walahwun waladdārul-ākhiratu khayrul lilladhīna yattaqūna afalā ta'qilūn

Na maisha ya dunia si chochte ila ni mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini? 32

Maelezo ya chini

32 Na huo uhai wa duniani walio uona makafiri kuwa ndio uhai wa pekee, na ambao hawaukusudii kwa kufanya vitendo vya kumridhi Mwenyezi Mungu, uhai huo si chochote ila ni mchezo usio kuwa na manufaa, na pumbao la kujipumbazia tu!! Na hakika nyumba ya Akhera ndio khasa uhai wa kweli. Huo unawanufaisha zaidi wale wanao mwogopa Mwenyezi Mungu na wanazifuata amri zake. Basi hamtii akilini jambo hili lilio wazi? Hivyo hamfahamu linalo kudhuruni na linalo kufaeni?