قُلۡ هَلُمَّ شُهَدَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ يَشۡهَدُونَ أَنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَ هَٰذَاۖ فَإِن شَهِدُواْ فَلَا تَشۡهَدۡ مَعَهُمۡۚ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمۡ يَعۡدِلُونَ ١٥٠
Qul halumma shuhadā'akumul-ladhīna yashhadūna annallāha harrama hādhā fa in shahidū falā tashhad ma'ahum walā tattabi' ahwā'al-ladhīna kaddhabū bi'āyātinā walladhīna lā yu'minūna bil-ākhirati wahum birabbihim ya'dilūn
Sema: Leteni mashahidi wenu watao shuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameharimisha hawa. Basi wakishuhudia, wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya walio zikanusha Ishara zetu, wala hawaiamini Akhera, na ambao wanamlinganisha Mola Mlezi wao na wengine. 150
Maelezo ya chini
150 Ewe Nabii! Waambie: Leteni wasaidizi wenu watakao kushuhudieni kwamba kweli Mwenyezi Mungu ameharimisha hivi mnavyo dai kuwa ni haramu. Wakihudhuria na wakashuhudia, basi wewe usiawasadiki, kwa sababu hao ni waongo. Wala usifuate matamanio ya hawa walio kanusha hoja za uumbaji na Qur'ani inayo somwa, na ambao hawaiamini Akhera nao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu, wanamfanya Yeye sawa na hao miungu inayo abudiwa kwa uwongo.