Surat Al-An'am, aya 151

6:151

۞ قُلۡ تَعَالَوۡاْ أَتۡلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمۡ عَلَيۡكُمۡۖ أَلَّا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗاۖ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُم مِّنۡ إِمۡلَٰقٖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكُمۡ وَإِيَّاهُمۡۖ وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَۖ وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ ١٥١

Qul ta'ālaw atlu mā harrama rabbukum 'alaykum allā tushrikū bihī shay'an wabil-wālidayni ihsānan walā taqtulū awlādakum min imlāqin nahnu narzuqukum wa iyyāhum walā taqrabul-fawāhisha mā zahara minhā wamā batana walā taqtulun-nafsal-latī harramallāhu illā bil-haqqi dhālikum wassākum bihī la'allakum ta'qilūn

Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini. 151

Maelezo ya chini

151 Ewe Nabii! Waambie: Njooni nikubainishieni yaliyo haramu ambayo inatakikana mshughulike nayo, na mjitenge nayo. Msimfanye yeyote kuwa ni mshirika na Mwenyezi Mungu, kwa shirki ya namna yoyote. Wala msiwafanye uovu wazazi wenu, bali wafanyieni wema mwisho wa wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya kukufikieni ufakiri, au mnao ogopa usikufikieni siku za usoni. Kwani nyinyi sio mnao toa riziki. Bali Sisi ndio tunakuruzukuni nyinyi na tunawaruzuku wao. Wala msikaribie uchafu wa uzinzi, kwani huo ni katika mambo mabaya yanayo katazwa, sawa sawa ikiwa jahara au kwa siri asiyo iona ila Mwenyezi Mungu. Wala msiuwe nafsi yoyote aliyo kataza Mwenyezi Mungu kuiuwa kwa kutokuwapo kupasa kwake, ila ikiwa kuuwa huko ni kwa haki ya kutekeleza hukumu ya mahkama. Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kwa amri ya nguvu muepuke haya yaliyo katazwa ambayo akili ya maumbile inakwambieni muepukane nayo, ili nanyi myatie akilini hayo.