Surat Al-An'am, aya 140

6:140

قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓاْ أَوۡلَٰدَهُمۡ سَفَهَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفۡتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِۚ قَدۡ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ ١٤٠

Qad khasiral-ladhīna qatalū awlādahum safahā bighayri 'ilmin waharramū mā razaqahumullāhuftirā'an 'alallāhi qad dallū wamā kānū muhtadīn

Hakika wamekhasirika wale ambao wamewauwa watoto wao kwa upumbavu pasipo kujua, na wakaharimisha alivyo waruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu. Hakika wamepotea, wala hawakuwa wenye kuongoka. 140

Maelezo ya chini

140 Hakika wamekhasiri hao walio wauwa watoto wao kwa ujinga na kwa mawazo ya uwongo, bila ya kujua nini matokeo ya kitendo chao, wala sababu yake; na wakajiharimishia nafsi zao riziki alizo waruzuku Mwenyezi Mungu katika mimea, na wanyama, huku wakimzulia Mwenyezi Mungu kwa kudai kuwa ni Yeye ndiye aliye harimisha. Na hakika wamejitenga mbali na Haki kwa sababu hiyo. Na kwa sababu ya uzushi huu hawakuwa katika wanao sifika kwa uwongofu.