Surat Al-An'am, aya 14

6:14

قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيّٗا فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَهُوَ يُطۡعِمُ وَلَا يُطۡعَمُۗ قُلۡ إِنِّيٓ أُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَسۡلَمَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ١٤

Qul aghayrallāhi attakhidhu waliyyan fātiris-samāwāti wal-ardi wahuwa yut'imu walā yut'amu qul innī umirtu an akūna awwala man aslama walā takūnanna minal-mushrikīn

Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. 14

Maelezo ya chini

14 Sema ewe Nabii! Mimi simfanyi yeyote kuwa ni mungu na msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu, Allah, tu. Yeye peke yake ndiye aliye ziumba tangu mwanzo mbingu na ardhi kwa nidhamu isiyo kuwa na kiigizo kilicho tangulia. Naye ndiye Mwenye kuwaruzuku chakula waja wake, wala Yeye hahitaji kwao chakula. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ameniamrisha niwe wa mwanzo wa kusilimu, na amenikataza kumshirikisha Yeye na yeyote mwenginewe katika kumuabudu.