وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدۡقٗا وَعَدۡلٗاۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ١١٥
Watammat kalimatu rabbika sidqan wa'adlal lā mubaddila likalimātihī wahuwas-samī'ul-'alīm
Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. 115
Maelezo ya chini
115 Na hakika hukumu ya Mwenyezi Mungu imekwisha toka. Basi maneno ya Mola wako Mlezi ya kweli na ya uadilifu yametimia kwa kuteremshwa Kitabu hichi Kitukufu, chenye kukusanya ukweli. Na ndani imo mizani ya kweli ya kupimia Haki na upotovu. Wala hapana wa kuyageuza maneno ya Mwenyezi Mungu na Kitabu chake. Naye Subhana ni Mwenye kusikia kila lisemwalo, Mwenye kukijua kila kinacho toka kwao.