Surat Al-Ahzab, aya 73

33:73

لِّيُعَذِّبَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ وَيَتُوبَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمَۢا ٧٣

Lliyu'addhiballāhul-munāfiqīna wal-munāfiqāti wal-mushrikīna wal-mushrikāti wayatūballāhu 'alal-mu'minīna wal-mu'mināti wakānallāhu ghafūrar rahīmā

Kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawaadhibu wanaafiki wanaume, na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na anawapokelea toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. 73

Maelezo ya chini

73 Ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanaafiki wanaume, na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na Mwenyezi Mungu apate kukubali toba za Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwingi wa rehema.