Surat Al-Ahzab, aya 55

33:55

لَّا جُنَاحَ عَلَيۡهِنَّ فِيٓ ءَابَآئِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآئِهِنَّ وَلَآ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ أَخَوَٰتِهِنَّ وَلَا نِسَآئِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُنَّۗ وَٱتَّقِينَ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا ٥٥

Llā junāha 'alayhinna fī ābā'ihinna walā abnā'ihinna walā ikhwānihinna walā abnā'i ikhwānihinna walā abnā'i akhawātihinna walā nisā'ihinna walā mā malakat aymānuhunna wattaqīnallāha innallāha kāna 'alā kulli shay'in shahīdā

Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala ndugu zao, wala watoto wa ndugu zao wanaume, wala watoto wa ndugu zao wanawake, wala wanawake wenzao, wala wale iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu. 55

Maelezo ya chini

55 Hapana dhambi kwa wakeze Nabii wakitojificha kwa baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au watoto wa ndugu zao wa kiume, au watoto wa ndugu zao wa kike, au wanawake Waumini wenginewe, au watumwa walio wamiliki, kwa sababu ya shida ya kuwahitajia kwa matumishi. Nanyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu katika mambo aliyo kuamrisheni, wala msipindukie mipaka yake. Kwani Yeye hakika anajua kila kitu, hapana kilicho fichikana kwake.