Surat Al-Ahzab, aya 51

33:51

۞ تُرۡجِي مَن تَشَآءُ مِنۡهُنَّ وَتُـٔۡوِيٓ إِلَيۡكَ مَن تَشَآءُۖ وَمَنِ ٱبۡتَغَيۡتَ مِمَّنۡ عَزَلۡتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكَۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن تَقَرَّ أَعۡيُنُهُنَّ وَلَا يَحۡزَنَّ وَيَرۡضَيۡنَ بِمَآ ءَاتَيۡتَهُنَّ كُلُّهُنَّۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَلِيمٗا ٥١

Turjī man tashā'u minhunna watu'wī ilayka man tashā'u wamanibtaghayta mimman 'azalta falā junāha 'alayka dhālika adnā an taqarra a'yunuhunna walā yahzanna wayardayna bimā ātaytahunna kulluhunna wallāhu ya'lamu mā fī qulūbikum wakānallāhu 'alīman halīmā

Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao, na umsogeze umtakaye. Na kama ukimtaka yule uliye mtenga, basi si vibaya kwako. Kufanya hivi kutapelekea yaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhi juu ya kile unacho wapa wao wote. Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. 51

Maelezo ya chini

51 Unaweza kumuakhirisha umtakaye katika kugawa zamu, na ukamjongeza umtakaye. Na kumtaka uliye muakhirisha zamu yake hapana lawama juu yako. Hivyo kuachiliwa utakavyo wewe yakaribia zaidi kupelekea furaha yao na baada ya kuwahuzunikia, na wao wote wawe radhi kwa ulio wapa. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo ndani ya nyoyo zenu, ya kuudhika au kuridhika kwa aliyo kufanyieni sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua yaliomo vifuani, Mpole hafanyi papara kuadhibu.