Surat Al-Ahzab, aya 40

33:40

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَآ أَحَدٖ مِّن رِّجَالِكُمۡ وَلَٰكِن رَّسُولَ ٱللَّهِ وَخَاتَمَ ٱلنَّبِيِّـۧنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا ٤٠

Mmā kāna muhammadun abā ahadim mir rijālikum walākir rasūlallāhi wakhātaman-nabiyyina wakānallāhu bikulli shay'in 'alīmā

Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. 40

Maelezo ya chini

40 Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu hata iwe ni haramu kwake kumwoa mt'alaka wake. Lakini yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni Mwenye kukhitimisha Manabii wote. Juu yake ni kufikilisha ujumbe kama alivyo muamrisha Mola wake Mlezi, bila ya kumchelea yeyote. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.