Surat Al-Ahzab, aya 26

33:26

وَأَنزَلَ ٱلَّذِينَ ظَٰهَرُوهُم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ مِن صَيَاصِيهِمۡ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعۡبَ فَرِيقٗا تَقۡتُلُونَ وَتَأۡسِرُونَ فَرِيقٗا ٢٦

Wa anzalal-ladhīna zāharūhum min ahlil-kitābi min sayāsīhim waqadhafa fī qulūbihimur-ru'ba farīqan taqtulūna wata'sirūna farīqā

Na akawateremsha wale walio wasaidia (maadui) katika Watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao; na akatia khofu katika nyoyo zao. Baadhi yao mkawa mnawauwa, na wengine mnawateka. 26

Maelezo ya chini

26 Na Mwenyezi Mungu aliwateremsha walio wasaidia makundi ya maadui katika Watu wa Kitabu, nao ni Mayahudi wa Bani Quraidha, kutokana na ngome zao walipo kuwa wakijilinda ndani yake. Na akaingiza katika nyoyo zao kitisho. Wengine mkawa mnawawauwa, nao ni wanaume, na wengine mnawachukua mateka, nao ni wanawake na watoto.