وَلَقَدۡ كَانُواْ عَٰهَدُواْ ٱللَّهَ مِن قَبۡلُ لَا يُوَلُّونَ ٱلۡأَدۡبَٰرَۚ وَكَانَ عَهۡدُ ٱللَّهِ مَسۡـُٔولٗا ١٥
Walaqad kānū 'āhadullāha min qablu lā yuwallūnal-adbāra wakāna 'ahdullāhi mas'ūlā
Na hakika walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kwamba hawatageuza migongo yao. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa. 15
Maelezo ya chini
15 Na hakika hawa wenye kukimbia kutoka midani ya vita walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kuwa watasimama imara katika vita pamoja na Mtume, na wala hawatakimbia. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa kwa yule mwenye kuitoa, na yampasa aitimize.