Surat Al-Ahzab, aya 11

33:11

هُنَالِكَ ٱبۡتُلِيَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَزُلۡزِلُواْ زِلۡزَالٗا شَدِيدٗا ١١

Hunālikabtuliyal-mu'minūna wazulzilū zilzālan shadīdā

Hapo ndipo Waumini walipo jaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali. 11

Maelezo ya chini

11 Katika wakati ule Waumini walifanyiwa mtihani juu ya kusubiri kwao juu ya Imani. Wakatikisika kwa khofu kwa mtikiso mkubwa.